Dstv Tanzania

MHASIBU MKUU CCM TAIFA ALLY MAKOA AMEKUTANA NA MAKATIBU WOTE WA CCM MKOA WA NJOMBE KUANZIA NGAZI YA TAWI MPAKA MKOA NA KUWAPA MUELEKEO WA NAMANA WA KUENENDA KATIKA NAFASI ZAO



PICHANI:Mhasibu Mkuu CCM Taifa Ally Makoe akiongea na  Makatibu wote wa chama wa ngazi ya kata na mawati.

Makoa  amepongeza Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe kwa kazi kubwa wanayo ifanya na kutoa viongozi bora katika Tiafa hili la Tanzania.
Hivyo amesema hana budi kuuita Mkoa wa Njombe ni Mkoa wa Kiuongozi kwani viongozi wengi wa Tifa hili wanatoka katika Mkoa wa Njombe.

Viongozi watendaji wamechaguliwa na wanachama na sasa wamepewa dhamana ya uongozi hivyo ni lazima kuwatumikia wanachama waliokuchagua

Mhasibu Mkuu amesema Chama kimekuja na makubaliano na makubaliano hayo yasipo fika kwa watendaji wakuu ambao ni makatibu wa kata na matawi makubaliano hayo hayatatekelezwa, hivyo ni lazima makatibu wa matawi na kata wayajue makubaliano hayo.

Mhasibu Mkuu wa CCM Taifa ametoa maelekezo katika mambo makuu matatu,

1.Mfumo wa mabadiliko wa kukusanya mapato ya chama.

Kila Wilaya itakuwa na akaunti moja ya kukusanyia mapato kuanzia ngazi ya tawi mpaka Wilaya, na ukusanyaji huo kwa sasa utamia Control namba ili kuweza kujua fedha iliyoingia inatoka katika tawi, kata ipi. Hivyo kila tawi au kata watachukua fedha ya matumizi kulingana na fedha ambayo wamekusanya. Mwisho amesema ikukmbukwe fedha hizo za kila kata au tawi zinazokusanya ni za wao wenyewe kata ua tawi kwani kwani wakitaka kutumia hawazuiliwi ila ni lazima zifuatwe taratibu za kutoa fedha .

2.Usajili wa wanachama

Usajili wa wanachama ndio agenda kuu katika chama cha Mapinduzi kwa wakati huu, hivyo amewaomba matibu wa Wilaya na kata kuhakikisha wananchi wanafikiwa katika matawi yao ili kuweza kuwapata.
 Hata hivyo Mhasibu Mkuu wa CCM Taifa amewapa Mashine  Makatibu wa Wilaya ya Makete na Ludewa ili kuongeza nguvu za kuandikisha wanachama kataika Wilaya hizo.


PICHANI: Mama Ngozingozi akimkabidhi fedha kiasi cha Shilini laki moja Mhasibu mkuu ili aweze kumkabidhi katibu wa CCM wanging'ombe kwa ajili ya kununulia Mashine kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kusajili wanachama 

Hali kadharika Mwanachama wa  CCM Rehema Ngozingozi (Mama Ngozingozi) amemchangia Katibu wa CCM Wilaya ya Wanging'ombe kwa ajili ya kununua Mashine nyingine ili kuweza kuongeza nguvu katika kendelea kuasajili wanachama

3.Kanuni za fedha.

Mhasibu Mkuu amewaomba matibu wote kununua vitatu vya kanuni za fedha ili waweze kujiongezea utaalamu katika kukusanya fedha, ktoa fedha na kutumia.

Mhasibu ameomba kila mtendaji wa chama akiweza anunue kitabu hicho cha kanuni za fedha kwani si gharama kubwa ili hali kinataratibu na kanuni zote za fedha.



PICHANI:Kushoto Mhasibu Mkuu wa CCM Taifa Ally Makoa akipanda Parachichi akiwa na katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima, baada ya kufanya kikao na  makatibu wote wa CCM toka ngazi ya Tawi mpaka Mkoa


Imetolewa na Ofisi ya  Katibu Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe
053580894























Hakuna maoni: