KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE AMEPONGEZA JITIHADA ZA KUBADILI AINA YA KADI ZA UANACHAMA MKOANI NJOMBE NA TANZANIA KWA UJUMLA
PICHANI:Katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole
Kufuatia chama cha Mapinduzi nchini Tanzania kubadilisha mfumo na aina ya kadi za uanachama.
Chama cha Mapinduzi Mkoani Njombe kimeanza zoezi hilo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako huku zoezi hilo likitajwa kuendelea katika maeneo yote Mkoani Njombe.
Akizungumza na Waandishi wa habari Katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole amepongeza jitihada kubwa zinazofanya wa CCM ndani ya chama na nje ya chama, amesema tayari Mkoa wa Njombe umeanza usajiri wa kadi hizo kwa mfumo mpya wa kielectronic ambapo kadi hizo zinatajwa kuwa msaada kwa wanachama kwani Kadi hizo zitawasaidia wanachama kuhifadhi taarifa zao mhimu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni