Dstv Tanzania

KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI CCM MKOA WA NJOMBE JOHNSON MGIMBA AFANYA UZINDUIZI WA KWAYA YA UVIKANJO YA MT.DONBOSCO PAROKIA YA LUGARAWA

PICHANI:Katibu wa Hamasa na Chipikizi CCM Mkoa wa Njombe Johnson Mgimba akizungumza na waumini wa Parokia ya Lugalawa

Leo Tarehe 11/11/2018 Katika Kanisa LA Mt Gabriel LA Parokia ya Lugarawa kwaya ya UVIKANJO Ilizinduliwa na Mgeni Rasmi Ndugu *JOHNSON ELLY MGIMBA KHC -Mkoa Njombe.*

Katika Ibada zote mbili za Leo kwaya hii ilipata kuhudumu Ishara ya kuanza Huduma Rasmi na Baadae Tafrija fupi ya Uzinduzi huu ilifanyika katika Ukumbi wa Veta Lugarawa.

Kwakuwa Kwaya ndio Inaanza walipata wasaa wakusoma Risala kwa Mgeni Rasmi lilikuwa na Changamoto za Kiuimbaji kama Kukosa Mwalimu,Sare,Vyombo vya Mziki,Chanzo cha mapato Kwa Kwaya.

Naye Mgeni Rasmi *Ndugu  Johnson Mgimba* Akijibu Risala Hiyo kwanza aliwapongeza kwakuanzisha kwaya hiyo ambayo anaambiwa ilikuwepo ila sasa ndio imerudi kwa upya ikiwa na kubatiza jina hilo LA Mt.Gabriel Alisema.

Aliendela Mgeni Rasmi kusema nao akasema  kwakuwa nikwaya inayoanza hivyo wasianze na Makubwa Ila   Kuna Mambo wanatakiwa kuanza nao kwa kipaumbele kwakuwa ndio wanaanza.

1.Waimarishe Uimbaji wao kwanza ambapo amewaagiza wamtafute Mwalimu na yeye atamgharimia malipo Mwalimu kwa kipindi atakachokaa nao kuwafundisha.

2.Kwakuwa ndio wanaanza Aliomba waendelee kufanya uinjilisti kwa Vijana wengine waendelee kujiunga na kwaya ambapo Amewaahidi kuwashonea sare wanakwaya wapya watakaoingia.

3.Kuhusu Chanzo cha mapato amewaagiza viongozi wakae chini wachambue waone nimradi UPI wanaweza kufanya na ukawaingizia Kipato wakishafanya wawasiline nae.

4.Kuhusu Vyombo Alisema kama alivyowaomba hapo kuu kuwa kwa sasa wasianze mambo mengi kwakuwa wanaweza jaribiwa hivyo aliomba kwanza watekeleze hayo hapo juu then wakishaona Uhai wao kama Kwaya ndipo atawasaidia namna ya kupita ili kuandaa Harambee kubwa ya Changizo ya unujuzi wa vyombo.

Mwisho Mgeni Rasmi alijitoa kuwa sehemu ya Walezi wao kwa muda wa Miaka miwili baada ya hapo anaamini watakuwa wamekuwa Tayari.

Mwisho aliwasihi Kanisa kwa ujumla kuwa msingi wa Taifa Imara upon mikononi Mwa Kanisa hivyo kanisa Lisimama kwenye nafasi yake Taifa halitayumba. Asema serikali ya awamu imekuja kwa wakati sahihi na nimpango wa Mungu tuiombee.
Picha ya Pamoja na waumini wa Parokia ya Lugalawa

Mwisho aliwaaga wakumbini na kurudi Njombe.





Hakuna maoni: